Luke 19:41-44

41 aAlipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, 42 bakisema, “Laiti ungalijua hata wewe leo yale ambayo yangeleta amani, lakini sasa yamefichika machoni pako. 43 cHakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. 44 dWatakuponda chini, wewe na watoto walioko ndani ya kuta zako. Nao hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukutambua wakati wa kujiliwa kwako.”

Isa Atakasa Hekaluni

(Mathayo 21:12-17; Marko 11:15-19; Yohana 2:13-22)

Copyright information for SwhKC